Thursday, September 4, 2014

HUYU NDIE NYANI ANAYEGAWA PESA HUKO NCHINI INDIA, MTAZAME HAPA

NYANI mmoja katika Jimbo la Himachal Pradesh, Kaskazini ya India, amewagawia watu pesa taslimu kutoka mtini.
Taarifa zinasema kuwa watu waliokuwa wanajivinjari katika mji wa Shimla jimboni humo, walianza kukimbia huku na kule wakiokota pesa zilizokuwa zinarushwa na nyani huyo kutoka juu ya mti kwa karibu saa moja.
Walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa nyani huyo kwa jina Simian aliiba fedha kiasi cha rupee 10,000 kutoka nyumba ya jirani katika eneo hilo.
Nyani huyo aliingia katika nyumba hiyo kutafuta chakula lakini alipokosa chakula akaamua kutoweka na pesa.
Jimbo la Himachal Pradesh limekuwa makao kwa wanyama wengi ambapo kuna takribani nyani 300,000
Nyani aina ya Macaque, huonekana kama wanyama wa kuabudiwa na hivyo hulishwa na wananchi.
Lakini katika miaka ya hivi karibuni wanyama hao, wamekuwa wakizozana na wakazi kwa sababu ya kuharibu mimea , kushambulia watu na hata kuwauma watoto.
Maofisa tayari wametangaza wanyama hao kuwa kero kubwa kwa wakazi wa jimbo hilo.
Nyani huyo mwanzo alionekana akiwa ameketi juu ya paa la nyumba akiwa na bunda la noti kabla ya kuanza kuwagawia watu pesa hizo kwa kuwarushia.
Watu walipoanza kukusanya pesa hizo, nyani huyo alikimbilia kwenye mti mwingine. Lakini watu waliokuwa wanaokota pesa hizo walimfuata kwani pesa haziachiki.
"Nyani alionekana kushutushwa na idadi ya watu waliokuwa wanamfuata lakini alipokimbilia kwenye mti mwingine, watu waliendelea kumfuata,'' alisema mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo.
HABARI: BBC