Thursday, September 18, 2014

KUTOKA IRINGA HILI NDILO JIWE LINASEMEKANA LILIKUWA LIKIZUNGUMZA #GANGILILONGA

8lngUkubwa wa jina Gangi lilonga linatokana na Jiwe linalopatikana Manispaa ya Iringa eneo la Gangi Lilonga ambalo kulingana na historia ya eneo hilo na simulizi za jiwe hilo ambalo linasemekana lilikuwa likiongea alikua akilitumia sana Mtemi Mkwawa.
Kwa miaka ya hivi karibuni jiwe hili halitumiki tena kwa imani hizi na kwa sasa limefanywa kama kivutio kwa watalii mbalimbali ambao wanafika kulishangaa,mambo ya Digital kwa sasa wanasema kuwa hakukua na sauti hizo za ajabu.
Kutokana na sehemu yenyewe kuwa mlimani inasemekana kuwa wazee walikua wanashindwa kujua kama ile ni Echo Sound yaani Mwangwi hivyo mtu anaweza kuongea kutoka mbali ukahisi jiwe ndilo linalozungumza.
Tafsiri ya jina hili Gangi Lilonga maana yake  GANGI(jiwe) LILONGA(linaloongea),Mzee Macha ni mwenyeji kidogo Mkoa wa Iringa uwepo wake zaidi ya miaka 30 anashare na sisi anayoyajua kuhusu jiwe hili.
Bonyeza play kumsikiliza.