Friday, September 19, 2014

MAKUBWA HAYA:MSANII WA FILAMU! LUNGI ETI ASIPOVAA KIHASARA, HAJISIKII RAHA

Lungi Mwaulanga ametoa kali baada ya kusema kuwa, bila kuvaa nguo zinazoanika baadhi ya sehemu zake ‘muhimu’ hasikii raha.
Msanii wa filamu bongo,Lungi Mwaulanga.
Akipiga stori na gazeti hili, Lungi alisema kutokana na hali ya joto ya Jiji la Dar, kuvaa nguo nyingi mwilini ni sawa na kujipa karaha hivyo hulazimika kuvaa vivazi vya kisasa zaidi.
”Najua kuna ambao wanakereka na uvaaji wangu lakini nadhani hawana sababu ya kukereka. Napenda kuvaa ninavyojisikia kwa hiyo hata nikivaaje, ni mimi na maisha yangu,” alisema Lungi.
ODAMA: NAANZAANZAJE KUMFICHA BWANA’NGU?
Stori: Rhoda joSIAH
Mwanadada anayeuza nyago kwenye filamu za Kibongo, Jennifer Kyaka ‘Odama’ amekanusha tuhuma ya kumficha mwandani wake na kufunguka kuwa, marafiki na familia yake wanamjua hivyo haoni sababu ya kumfanya kila mtu amjue.
Lungi Mwaulanga akiwa kwenye pozi.
Odama alikuwa akizungumzia madai ya kumficha mwanaume aliyezaa naye huku baadhi wakisema, hataki mtu yeyote amjue kwani ni mume wa mtu.
“Hivi naanzaanzaje kumficha mwandani wangu? Halafu nimfiche ili iweje? Ndugu na marafiki zangu wanamjua, wasiomjua wawe na subira, kila jambo lina wakati wake,” alisema Odama ambaye juzikati alinaswa akiwa ‘very close’ ukumbini na mwanaume aliyefahamika kwa jina la Daudi ambaye ni mume wa mtu.