Saturday, September 6, 2014

MSAFARA WA MAALIM SEIF WAPATA AJALI MBAYA..SOMA ZAIDI

Katibu wa CUF Wilaya ya Nyamagana, Rehema Mwenda amejeruhiwa na kupelekwa Hospitali ya Rufaa Bugando (kulia) na muonekano wa gari (kushoto) baada ya ajali katika wilaya ya Misungwi, jijini Mwanza.
Mkuu wa kitengo cha habari Wilaya, Mh Shido ambae pia ni Mwenyekiti wa Mtaa Utemini Kata ya Mirongo amejeruhiwa na kupelekwa Hospitali ya Rufaa Bugando.
Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamadi.
 Habari zinasema msafara wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamadi umepata ajali ukihusisha magari mawili ya msafara wa kiongozi huyo ambayo jumla yake yalikuwa saba yalipogongana na lori lenye tela.
 Akizungumza na mtandao huu, Mkurughenzi wa Habari wa CUf, Adam Kambaya alisema  Viongozi wawili wa CUF, katibu wa wilaya ya Nyamagana na mwenyekiti wa mtaa wa Nyamagana  ambao hakuwataja majina wamelazwa katika Hospitali ya Bugando kwa matibabu zaidi.