Thursday, September 18, 2014

UMEISIKIA HII?:UNAAMBIWA LILE BAO LA JAJA DHIDI YA AZAM LIMETUA ENGLAND TAYARI...EBU SHUKA NALO HAPA ILO BAO UJIONEE

Mshambuliaji wa Yanga, Geilson Santana ‘Jaja’ akishangilia goli. Na Wilbert Molandi
KWELI alichokifanya mshambuliaji wa Yanga, Geilson Santana ‘Jaja’ raia wa Brazil kupitia bao lake alilofunga dhidi ya Azam, si kitu kidogo.
Sasa baadhi ya mitandao, Watanzania na raia wengine kutoka katika nchi za Afrika Mashariki wanaoishi nchini England na Marekani, wamepata kipande cha video kinachoonyesha bao hilo alilolifunga wakati Yanga ikipambana na Azam FC katika mechi ya Ngao ya Jamii.
Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jaja alifunga mabao mawili lakini lile la pili ambalo ‘aliu-chop mpira, ndilo limekuwa gumzo zaidi.
Baadhi ya Watanzania na wengine mashabiki wa Yanga wanaoishi England, wamezungumza na Championi Jumatano na kusema Mbrazili huyo ni sehemu ya darasa kwa soka nchini.
“Nimepata ile ‘clip’ ya bao la huyo Mbrazili, kweli nimeshangazwa sana. Nafikiri ni bao la kwanza kali kufungwa kwenye ligi ya hapo nyumbani,” alisema Sospeter Michael ambaye anasomea biashara katika moja ya vyuo vya Mji wa Leicester.
Lakini Anthony Kitambi anayeishi katika jiji la pili kwa ukubwa England la Birmingham, amesema walikuwa wakilijadili bao hilo na baadhi ya rafiki zao kutoka Kenya na Uganda.
Kila mmoja amefurahishwa, kuna vitu vingi vya kujifunza. Angalia mfungaji alivyokuwa ametulia na uamuzi wake haukuwa ni wa kubahatisha.“Hiyo ndiyo sehemu ya kuonyesha kuwa soka linakua na waambie Watanzania wenzetu sasa wajifunze badala ya kufanya bao hilo ni sehemu ya soga tu,” alisema Kitambi.
Baadhi ya wapenda soka kutoka nchini Marekani, pia wameeleza kupitia mitandao mbalimbali kuhusiana na bao hilo kwamba ni mfano.Achana na England na Marekani, video ya bao hilo la Jaja imekuwa ikisambazwa sehemu mbalimbali na wadau kupitia Whatsapp.
Ukiiangalia utaona Jaja anaukimbilia mpira, halafu anatulia na ‘kumchungulia’ kipa Mwadini Ally, kabla ya kuukwamisha wavuni kwa ‘kuu-chop’.Kabla ya mabao hayo mawili dhidi ya Azam FC, mashabiki na wadau wengi wakiwemo wanaoipenda Yanga, walikuwa wakimbeza Mbrazili huyo kuwa ni mvivu na mzito