Thursday, October 16, 2014

ANGALIA PICHA ZA AJALI MBAYA YA GARI LA NG'OMBE ILIYOTOKEA LEO UBUNGO JIJINI DAR: CHEKI HAPA

MFANYABIASHARA mmoja wa mifugo (ng’ombe) na dereva waliokuwa katika lori lililokuwa limebeba mifugo hiyo, leo wamenusurika katika ajali iliyotokea asubuhi  eneo la Ubungo-Mataa,  jijini Dar es  Salaam.

Gari hilo lililokuwa limebeba ng’ombe wapatao thelathini likitokea  Wilayani Kondoa,  Dodoma, limepata ajali na ng’ombe kadhaa kuumia sehemu mbalimbali za miili .

Wakizungumza na mtandao huu, mashuhuda wamesema tukio hilo lilifuatia  mwendesha pikipiki (bodaboda) kukatiza kwa kasi mbele ya gari hilo na dereva alipoamua kuwakwepa, gari lilianguka.

Aidha mfanyabiashara wa mifugo hiyo, Abdalah Juma,  amelipongeza jeshi la polisi na askari kwa ulinzi  walioufanya hapo kwani hakuna kitu kilichopotea. 



Mfanyabiashara wa mifugo hiyo, Abdalah Juma,  akionyesha eneo la bega aliloumia katika ajali.
 
Gari lilivyokuwa baada ya ajali.  
Mifugo ikiwa kando ya barabara baada ya ajali.