MKURUGENZI wa Lino International Agency ambao ndiyo waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga amewaka kinomanoma baada ya kuulizwa habari za mrembo wake aliyejivua taji hivi karibuni, Sitti Mtemvu.
Lundenga alibwatuka maneno makali baada ya paparazi wetu kumuuliza juu ya uwepo wa taarifa kwamba shindano hilo linaweza kufungiwa kutokana na kashfa mbalimbali zinazolitafuna sambamba na ufafanuzi wa zawadi ambayo alipewa Sitti kama anaweza kuirejesha kwa mrembo namba mbili aliyechukua nafasi yake.
Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ndiyo waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga.
“Sikiliza nyinyi nawaheshimu sana sababu najua mpo makini, tusivunjiane heshima hizo habari zisizokuwa na kichwa wala miguu waachieni wanaokurupuka kuandika mambo ya uongo, wapuuzi sana wale,” alisema Lundenga na kukata simu na hata alipopigiwa tena, hakupokea.