Monday, November 24, 2014

MSUNGU WA BONGO MOVIE ANUSURIKA KIFO BAADA YA AJALI MBAYA YA GARI


Stori: Gladness Mallya
MSANII wa filamu Bongo, Stanley Msungu ‘Senetor’ amenusurika kifo baada ya kupata ajali na gari lake kuharibika vibaya.

Msanii wa filamu Bongo, Stanley Msungu ‘Senetor’.
Akipiga stori na gazeti hili, Msungu alisema anamshukuru Mungu kwani ungekuta sasa hivi ni maiti kwani ajali ilikuwa ni mbaya maeneo ya Bondeni, jijini Dar akielekea nyumbani kwake Tegeta ambapo gari lake alilokuwa akiliendesha aina ya Toyota Vits liliacha njia na kutumbukia mtaroni.
“Yaani ni Mungu tu kwani ungekuta sasa hivi watu wanazungumza mengine japokuwa ninasikia maumivu makali sana ya kifua na shingo pia gari limeharibika vibaya,” alisema Msungu.