Monday, November 24, 2014

MAPOKEZI YA MBUNGE DAVID KAFULILA BUNGENI LEO NOVEMBA 24 BAADA YA KUFUNGA NDOA

Kafulila-ndoa-pic2Siku ya Jumamosi Novemba 22 millardayo.com ilikupatia taarifa kuhusu Mbunge David Kafulila kufunga Ndoa Kigoma, leo Novemba 24 kaingia ndani ya Jengo la Bunge Dodoma na kupigiwa shangwe za mapokezi na Wabunge wa Bunge hilo wakati kikao kikiwa kinaendelea.
Spika wa Bunge Anne Makinda alikuwa kwa kwanza kuzungumza wakati Wabunge wakimpigia makofi David Kafulila alipokuwa anaingia; “… Bwana Harusi anaingia… Sasa Bibi Harusi yuko wapi mimi nilitegemea anakuwa pale… Mchezo mbaya huo.. Haya asante nashukuru, hongera…“- Anne Makinda.
Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia January Makamba naye aliongea haya; “… Na mimi napenda kuchukua fursa ya kumpongeza Mheshimiwa David Kafulila kwa kuoa, karibu kwenye klabu yetu na hongera sana… “
Bonyeza play hapa kusikiliza shangwe za mapokezi hayo Bungeni.