Tuesday, December 30, 2014

BAADA YA KUPATA KASHFA YA ESCROW MUHONGO AJISAFISHA KWA KUAGIZA UMEME BURE TARIME

Waziri wa Nishati na Madini, 
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameagiza kutolewa kwa umeme bure kwenye Kituo cha Ushirika wa Kutokomeza Ukeketaji kilichopo Kata ya Gorong’a, wilayani Tarime Mkoa wa Mara.
Kituo hicho hutoa elimu kwa wasichana kuhusu kupinga mila ya ukeketaji.
Waziri Muhongo alisema hayo alipotembelea kituoni hapo na vijiji mbalimbali kukagua mradi wa umeme vijijini.
Profesa Muhongo alisema kituo hicho hakitalipa gharama zozote za kuvutiwa umeme na kwamba Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) litawapa umeme bure ili uwasaidie kupata mwanga katika shughuli zao mafunzo.
“Nawashukuru kwa ubunifu wenu wa kuanzisha kituo hiki ili kuwasaidia wasichana waepuke kukeketwa... Tanesco itawapa umeme bure, nawaomba wasichana msome kwa bidii tena masomo ya sayansi na elimu mliyoipata iwajenge,” alisema.
Katika risala yao, wasichana hao walisema wamefika hapo kwa ridhaa ya wazazi wao, lakini wapo wasichana waliokimbia majumbani kukwepa kukeketwa.
Mkurugenzi wa kituo hicho, Sista Baibika alisema kuwa watu wapatao 634 kutoka Tarime na Serengeti wanaendelea na mafunzo hayo yaliyoanza Desemba 10 na yatahitimishwa Januari 5 mwakani.
Alisema elimu hiyo hutolewa kila mwaka katika kipindi hiki cha ukeketaji mkoani Tarime.