Tuesday, December 30, 2014

MSANII T-PAIN ATAPIGA SHOW KALI JIJINI MWANZA FEBRUARY 2015

Muimbaji wa Marekani, Faheem Rashad Najm maarufu kama T-Pain anatarajiwa kutumbuiza jijini Mwanza February mwakani.
T-Pain ambaye anafahamika kwa kufanya matumizi ya Auto-Tune kuwa maarufu kwenye muziki wa R&B duniani na aliyewahi kutamba na vibao vingi kama ‘I’m Sprung’ na ‘I’m N Luv (Wit a Stripper)’ atatumbuiza February 21 kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Show hiyo imeandaliwa kwa ushirikiano wa vituo vya redio vya Storm FM ya Geita na Jembe FM ya Mwanza.
Muimbaji huyo amewahi pia kushirikishwa kwenye nyimbo nyingi zilizotamba zikiwemo “I’m a Flirt” (remix) ya R. Kelly na T.I., “Outta My System” ya Bow Wow, “Baby Don’t Go” ya Fabolous, “I’m So Hood” ya DJ Khaled na wasanii kibao, “Shawty” ya Plies, “Kiss Kiss” ya Chris Brown, “Low” ya Flo Rida, na “Good Life” ya Kanye West.