Kuna taarifa kutoka nchini Uganda kuwa
Davido aliyepo nchini humo aliondoka kwenye
club ya jijini Kampala baada ya DJ kucheza
wimbo alioshirikishwa na Diamond, Number
One Remix.
Davido alikuwa akila bata kwenye lounge
iitwayo Laftaz ya jijini Kampala na baadaye
mood kukatika baada ya kusikia wimbo huo
ukichezwa. Mtandao wa BigEye Uganda
umeandika kuwa Davido aliyekuwa amepewa
kampani na msanii wa Uganda ambaye pia ni
mdogo wake na Jose Chameleone, Pallaso,
alirudi kwenye hoteli aliyokuwa amefikia.
Tumemtafuta Pallaso na haya ndio
aliyetuambia: I don’t know, I missed that
party, we were already partying and I was not
really paying attention so I don’t know,”
Pallaso alisema.
Hata hivyo Pallaso amekiri kusikia uvumi huo.
“ I heard some stories but you know there is a
lot of gossip going on in Kampala so you
could never know what to trust and what not
to trust, but I did not really see that par t,”
ameongeza.
Pallaso amemshirikisha Davido kwenye wimbo
wake utakaotoka wiki ijayo.