Staa wa Filamu za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ ameibuka na kusema kuwa kuelekea mwisho wa mwaka mastaa wengi wana Ukimwi na mbaya zaidi wanaambukizana wao kwa wao.
Akizungumza na gazeti la Ijumaa, Dude alisema kuwa mastaa wazima ni wa kuhesabika na kutaja sababu kubwa kuwa ni kubadilishana na kuibiana wapenzi bila kuwa na woga .
Aidha, Dude alisema anavyoona yeye ingeanzishwa kampeni ya mastaa wa Bongo kupima Ukimwi kwani anawahofia watoto wa kizazi kipya zaidi ambao wanajikuta wanaingia pabaya na kuzima ndoto zao.