Thursday, January 15, 2015

KESI YA CHID BENZ YAPIGWA KALENDA MPAKA JANUARI 21 MWAKA HUU

Mwanamuziki wa Hip hop nchini, Rashid Makwiro ’Chid Benz’ akiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar. (Picha na Maktaba Yetu)
KESI inayomkabili mwanamuziki wa Hip hop nchini, Rashid Makwiro ’Chid Benz’, imeahirishwa tena leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam mpaka Januari 21, mwaka huu.
Mwanamuziki huyo anakabiliwa na kesi ya kukamatwa na madawa ya kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar wakati akisafiri kuelekea mkoani Mbeya kwa ajili ya kutumbuiza mwaka jana.
Kesi hiyo imesomwa mbele ya Hakimu Waliarwanda Lema.