Mwanamke mmoja nchini Marekani ameuawa na mwanae wa kiume mwenye umri wa miaka miwili baada ya mtoto huyo kuishika bastola iliyokuwa kwenye mkoba wake na kujifyatua risasi kwa bahati mbaya.
Tukio hilo limemhusisha mwanamke mwenye miaka 29, Veronica J. Rutledge mkazi wa Blackfoot, Idaho nchini Marekani.
Kwa mujibu wa polisi, mtoto huyo alikuwa amekaa kwenye toroli la super market ya Walmart na kuingiza mkono kwenye pochi ya mama yake ambapo aliishika bastola iliyolipuka. Mwanamke huyo alikuwa akifanya shopping kwenye supermarket hiyo akiwa na wanae wanne.
Tukio hilo limenaswa kwenye video za ukaguzi kwenye supermarket hiyo na baadhi ya wafanyakazi walilishuhudia. Supermarket hiyo ilifungwa baada ya tukio hilo.