Friday, January 2, 2015

MWANAMUZIKI RIHANNA AAJIRIWA NA KAMPUNI YA PUMA

Mwanamuziki Rihanna
Msanii wa muziki nchini Marekani Rihanna anajiandaa kuanza kufanya kazi katika kampuni ya michezo Puma.
Ametangazwa kuwa mkurugenzi wa ubunifu wa vifaa vya kike na atakuwa uso wa vifaa vya mazoezi vya wanawake.
Rihana mwenye umri wa miaka 26 ataunda aina ya nguo zilizopo pamoja na viatu na kusaidia kubuni muundo mpya wa chapa cha bidhaa hizo.
Akizungumza kuhusu ushirikiano huo,Rihana amesema anafurahi kuona ni nini yeye na Puma wanaweza kubuni.
Wakuu wa kampuni ya Puma wanasema kuwa Rihana ataleta ubunifu katika ulimwengu wa riadha.
Nguo hizo mpya zitakuwa na mtindo wenye lengo la kuwaimarisha wanawake katika mazoezi mbali na kuwafanya kuamini miili yao pamoja na wao wenyewe.