Alafu ndo wenyewe mlikuwa mstari wa mbele kufunga maduka na kukimbia hovyo hovyo hata hao panya hamjawaona.
Ni aibu sana hii kwa mwanaume. Yaani badala ya kuhamasisha wanaume wenzenu mjitokeze kupambana na panyaroad, nyie ndio mnahamasisha watu wafunge biashara wakimbie!
dah aibu kweli hii. Ulegevu huu huwezi kuukuta huku Kanda ya Ziwa maana kwenye dharula kama hiyo huwa kuna vitu vifuatavyo wanaume mlipashwa kufanya:
Kupiga yowe na kukusanyika kwenda kuwafyekelea mbali hao panya Road.
Sasa basi ili muwe majasiri inabidi muache mambo ya kitoto kama:
Kunywa kahawa na kashata na joto lote lile.
Achaneni na kula pweza kuleni ugali wa mhogo na sangara.
Vitu kama ngisi, kachori na juice ya miwa vinawafanya muwe nare nare sana.
Ni aibu kwa mwanaume kuweka chumvi pilipili na ndimu kwenye mahindi ya kuchoma au
kuweka chumvi kwenye embe.
Acheni mara moja kula ubuyu mnajidharirisha mno.
Komeni kuangalia tamthiliya kwenye Haya ndio baadhi ya mambo yanawafanya muwe mdebwedo wa kutupa. Mkiendelea hivi ipo Siku panya road watakuja kuomba wawekewe maji ya kuoga na wake zenu mchana kweupe na nyie mpo. Jiangalieni sana...