Monday, February 23, 2015

BINTI WA MIAKA 27 AUAWA KWA KUKATWA MAPANGA.. WIVU WA KIMAPENZI WAHUSISHWA - SHINYANGA VIJIJINI

Mwili wa Marehemu Huma ukiwa
unachukuliwa na Maafisa wa Polisi
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa
jina la Huma Simon (27) mkazi wa
kitongoji cha Solwa Kata ya Solwa
Wilayani Shinyanga Vijijini ameuawa kwa
kukatwa mapanga na watu wasiojulikana
usiku wa kuamkia juzi.
Kwa mujibu wa Majirani Mwili wa
marehemu Huma umekutwa asubuhi
katika eneo la Shule ya msingi Solwa
ukiwa umekatwa mapanga sehemu
mbalimbali na kutelekezwa.
Taarifa zimesema Huma ambaye anaishi
na Mama yake Mzazi, alitoka usiku katika
chumba alichokua amelala na kumuacha
Mtoto wake wa kike anayekadiriwa kuwa
na miaka miwili, na kukutwa asubuhi
akiwa ameuawa.