Thursday, February 5, 2015

Hii ni taarifa ya idadi ya watu ambao hufariki kila siku kwa Saratani Tanzania


Wataalamu wa afya wamethibitisha kuwa saratani ni janga la kitaifa huku takwimu zaidi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa huo zikionyesha Watanzania wengi hupoteza maisha kila siku.
 
Mkurugenzi wa Taasisi ya Ocean Road Dk. Diwani Msemo wakati wa maazimisho ya siku ya saratani duniani alisema wengi wanaopata ugonjwa huo hufa kwa sababu wanakosa tiba, uhaba wa dawa na vifaatiba na pia wanachelewa kugundua iwapo wana ugonjwa huo.
 
Takwimu zilizoandikwa kwnye gazeti la Mwananchi zinaonyesha kuwa watu kati ya 80 hadi 100 hufariki kila siku.
 
Waziri wa afya Dk. Seif Rashid alisema asilimia 10 tu ndio wanaofika kutibiwa huku asilimia 80 wakiwa katika hatua za mwisho za ugonjwa huo.

Takwimu za kidunia zinaonyesha kuwa watu 8,000,000 hufa kila mwaka kwa saratani na hapa nchini watu 27,000 hufa kila mwaka huku 35,000 hugundulika ni wagonjwa.