Monday, February 2, 2015

MAZISHI YA BABA WA P-SQUARE KAMA SHEREHE

Acha kabisa! Mazishi ya baba wa mastaa wa muziki wa Nigeria, mapacha Peter na Paul Okoye wanaounda ‘Kruu’ ya P-Square, Moses Okoye aliyefariki dunia Novemba 24, 2014 yamekuwa kama sherehe, Ijumaa Wikienda limedodosa kilichojiri.
Mwili wa baba wa P-Square, marehemu Moses Okoye ukisindikizwa kwenye gari kwa tarumbeta.
Ishu hiyo ilijiri nyumbani kwa mastaa hao eneo la Ifitedunu, Jimbo la Anambra nchini humo Ijumaa iliyopita ikiwa ni siku 65 tangu mzee huyo alipofariki dunia baada ya kufanyiwa oparesheni ya goti alipodondoka kwenye ngazi nyumbani kwake maeneo hayo.
Wakina P-square wakiwa na wake zao katika msiba huo.
Tofauti na ilivyozoeleka kwamba kwenye msiba watu huwa wanalia na kuomboleza, mazishi hayo yaliyohudhuriwa na mastaa kibao nchini humo yalikuwa tofauti kwani watu walikuwa na nyuso za tabasamu huku wakiserebuka na matarumbeta juu.
Ulinzi mkali ukiimarishwa katika msiba huo.
Mbali na kuonekana kuwa kama sherehe, pia mazishi hayo yaliripotiwa kuwa ya gharama zaidi kuanzia jeneza lililobeba mwili wa baba yao, gari ‘spesho’ lililokuwa na jina la Dady badala ya namba za usajili na wahudhuriaji waliopiga sare nyeupe huku wakijifotoa picha wakicheka na kutupia kwenye mitandao ya kijamii.
Mwili wa baba wa P-Square ukiwa kwenye jeneza.
Pia kivutio kikubwa kilikuwa ni wake wa mastaa hao ambao walipewa ulinzi mkali uliowekwa katika mazishi hayo yaliyohudhuriwa kwa mualiko maalum.
Baba wa P-Square (aliyenyosha mikono) enzi za uhai wake.
Cha kushangaza, wakati mwili wa baba yao ukiwa mochwari, jamaa hao walidaiwa kuendelea na ratiba za kimuziki huku wakifanya shoo kama kawa jambo ambalo kwa Bongo haliwezekani.
Kwa sasa mastaa hao hawana mzazi hata mmoja baada ya mama yao naye kufariki dunia mwaka 2012