Tuesday, February 3, 2015

SUGE KNIGHT ASHITAKIWA KWA MAUAJI NCHINI MAREKANI

Suge Knight.
ALIYEKUWA mwanamuziki wa Rap nchini Marekani, Marion "Suge" Knight ameshitakiwa kwa mauaji na jaribio la kutaka kuua baada ya kumgonga mtu mmoja na gari lake hadi kumuua na baadaye kutoroka.
Eneo la Compton, Los Angeles ambapo Suge Knight aligonga mtu na kukimbia.
Iwapo itathibitika kuwa alifanya makosa hayo, Suge anaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.
Polisi wanasema kuwa Knight alijibizana na watu wawili wiki iliyopita katika eneo la kuegesha magari huko  Compton, Los Angeles na baadaye kumgonga mmoja wao huku mwingine akijeruhiwa vibaya.
Wakili wake anasema ilikuwa ajali na kudai kuwa mteja wake alishambuliwa na watu wawili.