Tuesday, February 3, 2015
Taarifa ya Startimes na TCRA kuhusu ukweli wa tatizo la ITV na EATV katika Startimes
Udaku Special-Leo mchana starmedia Tanzania iliitisha mkutano na waandishi wa habari kuzunguzia mambo mbalimbali sanasana kuhusu suala la ITV na EATV na sio kama ilivyotengenezwa na watu wa ITV. Mkutano huu ulihudhuriwa na waandishi mbalimbali wakiwemo ITV, STARTV, CHANEL TEN, TV1, CLAUD, SIBUKA, na vyombo vingine vya habari.
Pia mkutano huu ulihudhuriwa na wataalamu wa masafa kutoka TCRA. Taarifa hiyo ilikuwa kama ifuatavyo’
Taarifa kutoka kwa wataalamu wa STARTIMES
ITV na EATV zimekuwa zikionekana vibaya kwa watumiaji wa ving’amuzi vya STARTIMES kuanzia tarehe 27 january 2015, hali hii imekuwa ikisababisha usumbufu mkubwa sana kwa wateja wetu na umma kwa ujumla ambao wamekuwa wakifurahia chanel hizi katika vingamuzi vyetu. Wataalamu wetu walijaribu kufuatilia kwa ukaribu kujua tatizo katika mitambo yetu na wakagundua kwamba kulikuwa kuna mwingiliano wa mawimbi kutoka chanzo cha nje ‘WiMAX Operator’, hali hii ilitufanya sisi kama startimes kuwasiliana na mamlaka ya mawasiliano TCRA, kwani wao ndio wasimamizi wakuu wa masafa mbalimbali. Kuanzia tarehe hapo timu ya wataalamu kutoka STARTIMES na TCRA wamekuwa wakifanya kazi ya uchunguzi kujua ni ‘WiMAX operator’ gani ambaye amekuwa anasababisha hali hiyo. Katika uchunguzi uliofanywa na TCRA na STARTIMES ikagundulika yafuatayo
i. Kuna ‘WIMAX Operator’ mpya ambaye amekuwa akisababisha muingiliano huu katika dishi la STARTIMES linalopokea mawimbi ya ITV na EATV makongo
ii. ‘operator huyu amekuwa akirusha mawimbi yake katika masafa yenye ukubwa wa 3.598MHZ. Masafa haya yanakaribiana sana na masafa ya ITV/EATV dishi ambayo ni 3.644 na hivyo kusababisha muingiliano wa mawimbi hasa wakati wa jioni
iii. Nguvu ya mawimbi anayorusha ‘WIMAX operator’ huyu ni kubwa ukilinganisha na mawimbi tunayopokea katika kituo cha makongo
TCRA nao walizungumza kama ifuatavyo Tatizo la ITV na EATV katika vingamuzi vya STARTIMES limekuwa likisababishwa na muingiliano wa mawimbi na tayari tumegundua kuna ‘WiMAX Operator’. TCRA toka wiki lililopita tumekuwa tukifanya kazi kwa ukaribu sana na STARTIMES kuweza kujua chanzo cha tatizo na kutatua tatizo
HITIMISHO
Tunaamini kwamba kutokana na taarifa iliyotolewa na wataalamu wetu na wataalamu wa TCRA ni ukweli kwamba tatizo hili halijasababishwa na STARTIMES kama ilivyoelezwa awali na ITV katika taarifa zao za Habari. Mara zote startimes imekuwa ikifanya kila liwezekanalo kuhakikisha watanzania wanapata chanel zote za nyumbani Hivyo basi tumesikitishwa na taarifa zilizotolewa ITV na ambazo hazikuwa na uchunguzi wowote toka pande husika na kusababisha usumbufu kwa wateja wtu.
Starmedia Tanzania