Friday, March 27, 2015

LEO NIMEPITA BUGURUNI NA KUKUTA HALI HII.. HATUA ILIYOFUATA BAADA YA ISHU YA MAFURIKO

IMG_4572
Matatizo yaliyojitokeza kutokana na ishu ya mvua kubwa kunyesha DAR bado yanaendelea kuonekana, leo ripota wa millardayo.com kapita maeneo ya Buguruni na kukuta mashine zikiwa zimefunga katika eneo ambalo lilikumbwa na mkasa wa mafuriko pia.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi alikuwepo eneo hilo akishuhudia kuendelea kwa shughuli hiyo ambapo amesema Serikali imeamua kuwasaidia watu waliokumbwa na mafuriko eneo hilo kwa kuweka mashine hizo ambazo zimekuwa zikitoa maji katika eneo hilo kwa siku ya tatu mfululizo.
IMG_4582
Mkuu huyo wa Wilaya amesema Serikali itafanya tathmini ya nyumba za watu walio katika eneo hilo ili iwalipe fidia wahame kutokana na eneo hilo kukumbwa na mafuriko kutokana na bomba la kutolea maji taka kuziba.
IMG_4592
IMG_4617
IMG_4621
IMG_4659