Mrembo aliyewahi kushiriki Kinyang’anyiro cha Miss Tanzania 2005/06, Maureen Gislary, hivi karibuni amenaswa usiku akijisaidia haja ndogo barabarani (kuchimba dawa) huku akiwa hana wasiwasi.
Ilikuwa mida ya saa 7 usiku maeneo ya Magomeni jijini Dar ambapo mrembo huyo alionekana kuzidiwa na kuamua kufanya hivyo huku baadhi ya watu wakimpiga chabo.
Hata hivyo, baada ya kumaliza haja yake, Maureen alinyanyuka na kurudi alipokuwa amekaa na kuendelea kunywa pombe.
Mwandishi wetu alipomfuata na kumuuliza imekuwaje amefanya kitendo kile kisicho cha kistaarabu, hakutoa ushirikiano.