Thursday, April 2, 2015

BREAKING NEWS!!! CHUO KIKUU CHA GARISSA NCHINI KENYA CHASHAMBULIWA NA MAGAIDI

140718522
Wapiganaji waliofunika nyuzo zao wameshambulia eneo la chuo kikuu cha Garissa kazkazini mwa Kenya karibu na mpaka wa taifa hilo na Somali.Milio mikali ya risasi pamoja na milipuko imesikika katika chuo kikuu cha Garissa mjini humo.
Maafisa wa usalama wa Kenya wamethibitisha kuwa watu wawili wamefariki huku wanne wakijeruhiwa.
Wakaazi wa eneo hilo wametakiwa kukaa mbali na eneo la chuo hicho.
Haijulikani ni ni nani aliyekusika na shambulizi hilo ,lakini kundi la wapiganaji wa Somalia Al shabaab limetekeleza misururu ya mashambulizi mjini Garissa pamoja na maeneo mengine ya Kenya tangu mwaka 2011.