Sunday, April 12, 2015

DIAMOND: NILIWAHI KUPENDWA NA MSICHANA BAADA YA KUJIFANYA MIMI NI Z-ANTO


Diamond Platnumz na meneja wake, Babu Tale jana walikuwa wakihojiwa kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM na kupitia Heka Heka alishare mambo mengi ambayo watu hawayafamu.


Muimbaji huyo alidai kuwa kabla hajatoka kwenye muziki, alikuwa anapenda sana kuimba wimbo wa Z-Anto, ‘Binti Kiziwi’ kiasi cha watu wengine kuamini yeye ndio Z- Anto.

Alisema ikatokea msichana mmoja akampenda akijua anayempenda ni Z-Anto lakini baada ya video ya wimbo huo kutoka, watu wakamjua kwamba sio yeye.

Anadai kuwa baada ya kujulikana ukweli huo, ilibidi asiendelee kukatiza maeneo ya Kariakoo aliyokuwa akiyatumia kukaa mara nyingi na kumchukua wiki tatu bila kwenda huko.

Alisema siku alipokutana na binti huyo aliyempenda kwa kudhania ni Z-Anto, alibadilisha njia fasta kwa kuhofia kuumbuka!

Swali je kwasasa Z- Anto amefulia wapi?