Sunday, April 12, 2015

Shamsa Ford: Nay ni Mwanaume wa Ndoto za Wanawake Wengi...Ila zamani Nilikuwa Simpendi!

Staa wa Bongo Movies, Shamsa Ford amemmwagia sifa  Staa wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego kuwa hakuwahi kujua kama ni mkarimu huku akidai kuwa anafaa kuwa mume! 
Shamsa ambaye aliachana na mume wake tangu October mwaka jana, ameiambia Bongo5 kuwa aliombwa na Nay ashirikishwe katika filamu yake.
 
Sisi ni washkaji sema Nay ana kazi yake ya filamu ndio akaona mimi ndo nafaa, Hakuna kitu chochote zaidi ya kazi,” amesema Shamsa.
 
Kabla ya kupata nafasi ya kuongea na Nay nilikuwa namuona ni mtu fulani mgomvi mgomvi, in short nilikuwa simpendagi! Kama unakumbuka aliwahi kutuponda Bongo Movie na mimi kuna siku nilihojiwa na kituo kimoja nikamponda sana! Lakini nimekuja kukutana na Nay nimegundua ni mtu tofauti sana. Sasa hivi mimi namzungumzia Emmanuel is man ambaye kila mtu au kila mwanamke anaweza akamhitaji kuwa naye! Ana huruma ana upendo, he is a good man, kama nilivyosema mwanamke yoyote atapenda kuwa naye. Kwahiyo ni husband material,” aliongeza Shamsa.
 
Kwa upande mwingine, Shamsa amewataka mashabiki wa kazi zake kutambua kuwa yeye ni mtu mzima na ana maamuzi ya kufanya kile anachokipenda ili mradi asiharibu kazi.
 
Mashabiki wangu wajue Shamsa mimi najielewa najitambua ni mkubwa na ninajua zuri na baya,” amesisitiza muigizaji huyo. “Wasinihukumu kwa ambacho wanakiona au wanachokisikia, wanisubiri mimi kama mimi Shamsa na hayo wanayoyasikia hayawezi kuniharibia mimi kazi zangu au kuachana mimi na mume wangu ndo nitashuka kisanii, hapana! Wasihukumu hivyo, mimi nipo makini na kazi zangu.”