MSHAMBULIAJI wa zamani wa kimataifa wa Zanzibar, Mcha Khamis amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Baba huyo wa kiungo wa Azam FC na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Khamis Mcha ‘Vialli’ amefariki duniani mjini Dar es Salaam ambako alikuwa anapatiwa matibabu.
Enzi za uhai wake, Mcha mkubwa alichezea klabu za KMKM na Miembeni pamoja na timu ya taifa ya Zanzibar. Pumzika kwa amani Mcha Khamis, ahadi yako imetimia.