Friday, April 3, 2015

MOSHI WASABABISHA AJALI MBAYA MKWAJUNI JIJINI DAR

Umati wa watu ukijaribu kuokoa abiria waliokuwemo.
Gari lililokuwa likitokea Kawe kuelekea Kariakoo likiinuliwa.
Mwonekano wa gari lililodaiwa kutoa moshi na kusababisha ajali.
Waokoaji wakimtoa abiria aliyebanwa na vyuma.
Shughuli ya uokoaji ilivyokuwa.
Majeruhi akipelekwa kupata msaada.
Mwonekano wa gari lililokuwa likitokea Makumbusho kuelekea Temeke.
MAGARI mawili yanayosafirisha abiria jijini Dar es Salaam, leo yamegongana katika ajali iliyotokea eneo la Mkwajuni na kujeruhi vibaya abiria wake.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema ajali hiyo imesababishwa na gari lililokuwa linatokea Kawe kuelekea Kariakoo lililokuwa linafuka moshi na kusababisha  njia nzima kujaa moshi na hivyo kusababisha magari hayo kugongana na kuangukia bondeni.
Chanzo kutoka eneo la ajali kimesema majeruhi wengi wamepelekwa hospitali ya Mwananyamala na Muhimbili ambapo hali zao zilikuwa hazijulikani wakati mwandishi wa mtandao huu akitoka eneo la tukio.