Basi la Burudani likionekana mara baada ya ajali hiyo kutokea huko eneo la Soni, jimbo la Bumbuli Mkoani Tanga jana.
Habari ambazo zimeweza kupatikana ni kuwa zaidi ya abiria 50 wamenusurika kifo baada ya basi lao lililojulikana kwa jina la Burudani, kugongana uso kwa uso na Lori la tenki la mafuta maeneo ya Soni katika jimbo la Bumbuli, mkoani Tanga.
Kwa mujibu wa taarifa hizo ni kuwa, ilielezwa kuwa Lori la mafuta lilikata breki na kuvaana na basi hilo uso kwa uso. Kwenye ajali hiyo hakuna kifo ila inaelezwa kuwa abiria kadhaa wamejeruhiwa na wamekimbizwa Hospitali. Tutaendelea kukuletea taarifa zaidi kila zinapopatikana kutoka vyanzo mbali mbali vya habari popote pale na kukujuza hapa zikiwa zimehaririwa na kukufikishia wewe msomaji wetu.