Sunday, May 24, 2015

KIONGOZI WA CHAMA CHA UPINZANI BURUNDI AUAWA

Baadhi wananchi wakiwa eneo alipouawa Zedi Feruzi.
KIONGOZI wa chama kidogo cha upinzani nchini Burundi ameuawa kwa kupigwa risasi katika Mji mkuu wa nchi hiyo Bujumbura.
Mwili wa Zedi Feruzi amabye alikuwa kiongozi wa Chama cha Union for Peace and Development ulipatikana nje ya nyumba yake kwenye mji wa Bujumbura.
Juzi Ijumaa watu wawili waliuawa katika maandamano hayo yaliyochukua wiki kadhaa huku watu zaidi ya 100,000 wakiwa wameihama nchi hiyo kutokana na vurugu hizo za kupinga uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu.