BAADA ya wiki kadhaa kupita tangu picha zake zisambae zikimuonesha gauni likiwa limevuka nakuachia ‘nido’ wazi, staa wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameibuka na kuwaomba radhi kinamama wote.
Akipiga stori na Over The Weekend, Shilole alisema kuwa anajua kwamba kitendo hicho kimewakwaza wengi na hakukusudia kufanya jambo kama lile. “Nimejifunza mengi na naendelea tena kuomba msamaha kuwa tatizo hili halitajitokeza tena ,niwaombe radhi kina mama na mashabiki wangu,” alisema. Shilole alifanya tukio hilo alipokuwa jijini Antwepen, Ubelgiji kwenye shoo ambapo aliongozana na mpenzi wake,Nuh Mziwanda.