Klabu ambayo haitakamilisha mchakato huo haitaruhusiwa kushiriki ligi kuu ifikapo msimu wa 2015/16. Simba na Yanga ni klabu kongwe katika Ligi Kuu, ambazo zinaweza kukumbwa na adhabu hiyo zisipotekeleza agizo hilo.
Wachezaji wa klabu kongwe, SImba (jezi nyekundu) na Yanga SC (jezi za njano) wakisukumana katika moja ya mechi zao |
Katika hatua nyingine, kutokana na maamuzi ya mkutano mkuu wa TFF uliofanyika Morogoro ambao uliagiza wanachama wake wapya wapewe kompyuta, agizo hilo limetekelezwa na kompyuta hizo watakabidhiwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji wanaotoka kanda hizo ili waziwakilishe maeneo husika. Mikoa hiyo ni Geita, Katavi, Manyara, Njombe na Simiyu.