Wednesday, May 27, 2015

UTAJIRI WA MBWANA SAMATTA NI KUFURU.

Moja  ya magari ya heshima duniani ni Ranger Rover.
Wachezaji wengi maarufu duniani kote wanatembelea aina hii ya magari na hupenda kwenda nayo mazoezini.
Ranger Rover ziko za  'Modeli' tofauti, lakini asikwambie mtu, ni raha na heshima kuendesha aina hii ya gari mjini.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ame-posti picha kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram akiwa ameegemea gari ya thamani aina ya Range Rover.
Katika picha hiyo Mbwana ameandika maneno akieleza kwamba picha haina maelezo mengi kwababu akiyaweka anaweza kuharibu, lakini akasisitiza kuwa picha inatoa somo kwa wachezaji uzao wa sasa katika soka la Tanzania.
Stori ya kufurahisha ipo mwishoni kabisa ambako ameweka  maneno haya;
NB: Nishaacha toka 2012 kupiga picha Kwenye magari ya watu
Tafsiri ya maneno haya ni kwamba toka mwaka 2012 mpaka sasa, Samatta anapiga picha kwenye magari yake tu. Kwa maana hiyo Range Rover (pichani chini) ni yake.
Hiyo ilikua ni post ya Mbwana Samata  akiwa mbele ya Range Rover yenye namba ya Tanzania ndani ya DR Congo.
 Sasa hizi ni taarifa ambazo hauzijui kuhusu Mbwana Samata.
Mbwana ana magari saba likiwemo Range Rover  hilo hapo juu
Vyanzo vyangu vya habari vimesema kwamba amenunua kwa Tsh milioni 80. 
Pia Mbwana ana nyumba tano hapa Tanzania. 
Huu ni mfano wa kuigwa kabisa na hivi vitu viwe mfano kwa kila kijana mwenye malengo na maisha yake na sio wachezaji mpira tu. Hakuna cha kukuzuia kufika malengo yako.