Neema! Baadhi ya mastaa wa tasnia mbalimbali Bongo, wamefunguka kuwa kipindi hiki cha uchaguzi, kwao ni msimu wa kutengeneza hela kutoka kwa wagombea kama watahitaji huduma yao ya burudani.
Kwa mujibu wa baadhi ya wasanii, wao wapo au watakuwa tayari kuwapigia kampeni wagombea hao ilimradi tu wanavuta mshiko wa maana.
KULWA KIKUMBA ‘DUDE’:
Huu ndiyo msimu wa kulamba hela kutoka kwa wagombea. Mimi ni mtoa huduma kama zilivyo huduma nyingine, kuhusu kuwa timu au mfuasi wa mtangaza nia si kweli, yeyote akinihitaji niko tayari kwa huduma ya kisanaa.
NASIBU ABDUL ‘DIAMOND
Muziki ni biashara na ni kazi au huduma kama zilivyo huduma nyingine, kwa hiyo inapotokea mtu anahitaji huduma yangu nipo tayari kumpatia kama atatimiza masharti yangu kwa maana ya mkwanja. NICKSON SIMON ‘NIKKI II:
Mimi muziki ni kazi, wote ni viongozi wangu ninaowaheshimu kwa dhamira zao za kutangaza nia na ninaenda kwao kama mtoa huduma, kama huduma nyingine zinazowafuata wateja wao lakini kuhusu la kuwa mwanachama au mfuasi wa mtangaza nia, hiyo ni siri yangu.
Hivi karibuni, baadhi ya mastaa walishuhudiwa wakiwa ‘bize’ kwenye mikutano ya watangaza nia kwa nafasi ya urais, hasa kwa makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kama kwa Edward Lowassa (Arusha) na Bernad Membe (Lindi).