Sorry! Staa wa sinema za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’ anadaiwa kumwangukia mumewe, Abdallah Shakoor ili kurejesha uhai wa ndoa yao ‘iliyokwaruzwa na makucha ya shetani’ ikiwa ni njia ya kurudisha heshima na hadhi yake kwenye familia na jamii kwa jumla.
Habari kutoka kwa chanzo makini kilieleza kwamba, mara kadhaa Davina amekuwa akiomba msaada kwa ndugu, jamaa na marafiki wamsaidie kumuombea msamaha kwa mumewe ili waendelee na maisha kama ilivyokuwa awali.
“Davina amekubali yaishe, unajua anampenda sana mumewe, ‘so’ anahaha kwa ndugu ili wamuombee msamaha,” alisema ‘kikulacho’ huyo wa Davina.
Baada ya kuudaka ‘ubuyu’ huo, Ijumaa Wikienda lilizungumza na Davina ambapo alikuwa na haya ya kusema: “Hayo ni maisha yangu binafsi, hayamhusu mtu, kwanza nipo kwenye kikao, niache.”