Thursday, June 25, 2015

NACTE YAVIFUTIA USAJILI VYUO VITATU (3) NA KUVISHUSHA HADHI VYUO KUMI NA SITA (16)‏..BOFYA HAPA KUVIJUA USIJE UKAINGIA MKENGE

001.DRKaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi(NACTE)Dkt. Adolf Rutayuga(katikati)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam(hawapo pichani)wakati wa kutangaza ubora wa elimu ya ufundi inayotolewa na baraza hilo.Baraza hilo limevifuta usajili vyuo vitatu na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita.Kushoto ni Mkurugenzi wa Mitaala wa baraza hilo Twilumba Mponzi na Msaidizi wa katibu Mtendaji Alex Nkondola.
002.DRWakurugenzi wa Manejimenti ya NACTE wakiwa kwenye mkutano pamoja na waandishi wa habari uliohusu kutangaza ubora wa Elimu ya ufundi inayotolewa na baraza hilo lilitangaza kuvifutia usajili vyuo vitatu na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita.
004.DRMwandishi wa habari kutoka kituo cha EAT, Noah Laltaila akimuuliza swali Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi(NACTE)Dkt. Adolf Rutayuga kwenye mkutano uliohusu kutangaza ubora wa Elimu ya ufundi inayotolewa na baraza hilo lilitangaza kuvifutia usajili vyuo vitatu na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita.
005.DRBaadhi ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye mkutano wa Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi(NACTE) uliohusu kutangaza ubora wa elimu unaotolewa na baraza hilo.Baraza hilo limevifuta usajili vyuo vitatu na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita.
HOTUBA YA KAIMU KATIBU MTENDAJI WA BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE) DKT ADOLF B. RUTAYUGA KUHUSU TAMKO LA BARAZA LA KUVIFUTIA USAJILI BAADHI YA VYUO NA KUVISHUSHA HADHI VINGINE – 24/06/2015
Ndugu waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, ninayo furaha kubwa kuwakaribisha katika ofisi za Baraza. Lengo la kuwaita hapa leo ni kuwapa taarifa juu ya maamuzi yaliyofikiwa na Baraza ikiwa ni katika jitihada za kuinua ubora wa elimu ya ufundi nchini.
Ndugu Waandishi wa Habari
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura ya 129, kwa lengo la kusimamia na kuratibu taaluma zinazotolewa na taasisi na vyuo vva elimu ya ufundi nchini, ambavyo siyo vyuo vikuu au vyuo vikuu vishiriki. Jukumu kubwa la Baraza ni kuendeleza na kuinua ubora wa elimu ya ufundi nchini kwa kusimamia kikamilifu shughuli za kuendesha mafunzo ili tuzo zinazotolewa na taasisi na vyuo ziwe na ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa.
Kwa kutumia Sheria na Kanuni za Baraza za Usajili (2001) na zile za Ithibati na Utambuzi (2001), mnamo tarehe 20 Februari 2015, Baraza lilitoa notisi ya siku 30 kwa taasisi na vyuo vilivyokiuka taratibu na vyenye mapungufu makubwa ya Usajili na Ithibati kupitia taarifa yake kwa Umma. Notisi hii ililenga kuzipa taasisi na vyuo nafasi ya kujirekebisha.
Baraza linakiri kuwa taasisi na vyuo vingi kama vilivyoorodheshwa kwenye Jedwali Na. 1, Jedwali Na. 3, na baadhi kwenye Jedwali Na. 5 vimechukua hatua mbalimbali za kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza. Hata hivyo, hadi kufikia leo tarehe 24 Juni 2015 yaani siku 124 baada ya Notisi ya Baraza, kuna vyuo ambavyo havijachukua hatua yoyote ya kurekebisha mapungufu yake kama inavyooneshwa kwenye Jedwali Na. 2 na Jedwali Na. 4.
Tamko la Baraza
Kutokana na mapungufu hayo Baraza limeamua kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zake kwa taasisi na vyuo vyote vilivyoorodheshwa katika Jedwali Na. 2 na Jedwali Na. 4 kwa makosa yafuatayo:
  1. a)    Ama kumalizika kwa muda wa  Usajili wa Awali (Preparatory Registration) na Usajili wa Muda (Provisional Registration); au
  2. b)    Kutoanza mchakato wa kupata Ithibati baada ya kupata Usajili Kamili; au
  3. c)    Kumalizika kwa muda wa Ithibati na kutochukua hatua ya kuomba upya Ithibati (re-affirmation); na
  4. d) Taasisi na Vyuo kuamua vyenyewe kusitisha kutoa mafunzo kwa sababu mbalimbali.
Jedwali Na. 1: Taasisi na Vyuo vinavyoruhusiwa kuendelea na taratibu za Usajili baada ya kutimiza masharti
Na
Jina la Chuo/TaasisiNamba ya Usajili
1Regional Aviation College – Dar es SalaamREG/EOS/028P
2Zoom Polytechnic College – Dar es SalaamREG/EOS/030P
3Gataraye Research and Training Centre – Dar es SalaamREG/EOS/034P
4Modern Commercial Institute (MCI) – Dar es SalaamREG/BMG/024P
5Evin School of Management – Dar es SalaamREG/BMG/026P
6Agape School of Management – Dar es SalaamREG/BMG/027P
Jedwali Na. 2: Taasisi na Vyuo vilivyofutiwa Usajili na kuzuiliwa kudahili wanafunzi wapya baada ya kutotimiza masharti ya Usajili
Na.Jina la Chuo/TaasisiNamba ya Usajili/Maelezo
1Dar es Salaam College of Clinical Medicine – KinondoniUsajili wa Awali
2Ndatele School of Medical Laboratory Sciences – Dar-es-SalaamUsajili wa Awali
3Institute for Information Technology – Dar es SalaamREG/EOS/014
4DARMIKI College of Educational StudiesHakijasajiliwa. Kimezuiliwa kudahili wanafunzi
Jedwali Na. 3: Taasisi na Vyuo vinavyoruhusiwa kuendelea na taratibu za Ithibati baada ya kutimiza masharti
Na.Jina la Taasisi/ChuoNamba yaUsajiliHadhi Kabla yaNotisiHadhi Baada yaNotisi
1Mabughai Community Development Technical Training Institute – LushotoREG/EOS/040Usajili KamiliUsajili Kamili
2Kizimbani Agricultural Training Institute – ZanzibarREG/ANE/027Usajili KamiliIthibati ya Awali
3Civil Aviation Training Centre – Dar es SalaamREG/EOS/006Ithibati ya MudaIthibati ya Muda
4Ardhi Institute – TaboraREG/EOS/010Ithibati ya MudaIthibati Kamili
5Bandari College – Dar es SalaamREG/EOS/018Ithibati ya AwaliIthibati ya Awali
6Tanzania Institute of Rail Technology – TaboraREG/EOS/012Ithibati ya AwaliIthibati ya Awali
7RETCO Business College (RBC) – IringaREG/BMG/025Usajili KamiliUsajili Kamili
8Aseki Business School – DodomaREG/BMG/030Usajili KamiliUsajili Kamili
9Western Tanganyika College – KigomaREG/BMG/032Usajili KamiliUsajili Kamili
10Law School of TanzaniaREG/BMG/040Usajili KamiliUsajili Kamili
11Royal College of Tanzania  (RCT) – Dar es SalaamREG/PWF/004Ithibati ya AwaliIthibati ya Awali
12Tanzania Regional  Immigration Training Academy  (TRITA) – MoshiREG/PWF/030Ithibati ya AwaliIthibati ya Awali
13Morogoro School of Journalism (MSJ) – MorogoroREG/PWF/005Ithibati ya MudaIthibati ya Muda
14Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBa) – Bagamoyo (former Bagamoyo College of Arts – Bagamoyo)REG/PWF/010Ithibati KamiliIthibati Kamili
15Newman Institute of Social Work (NISW) – KigomaREG/PWF/016Ithibati KamiliIthibati Kamili
16Njuweni Institute of Hotel, Catering & Tourism Management – KibahaREG/ANE/016Ithibati ya AwaliIthibati ya Awali
17Geita School of Nursing – GeitaREG/HAS/079Ithibati ya AwaliIthibati ya Awali
18St. Gaspar Nursing School – ItigiREG/HAS/090Usajili KamiliUsajili Kamili
19Bugando School of Nursing – MwanzaREG/HAS/052Ithibati ya AwaliIthibati ya Awali
20COTC Mafinga – IringaREG/HAS/047Ithibati ya AwaliIthibati ya Awali
21Kagemu School of Environmental Health  Sciences – BukobaREG/HAS/034Ithibati ya AwaliIthibati ya Awali
22Mvumi Institute of Health Sciences – DodomaREG/HAS/011Ithibati ya AwaliIthibati ya Awali
23Tanzania Training Centre for International Health – IfakaraREG/HAS/003Ithibati ya MudaIthibati ya Muda
24Mbeya Polytechnic College (former Ilemi Polytechnic College) – MbeyaREG/BMG/031Usajili KamiliUsajili Kamili
25Institute of Sports Development Malya – MwanzaREG/PWF/019Usajili KamiliUsajili Kamili
26Ruaha Community Development Training Institute (CDTI) – IringaREG/PWF/028Usajili KamiliUsajili Kamili
27Uyole Community Development Training Institute (CDTI) – MbeyaREG/PWF/027Usajili KamiliUsajili Kamili
28Institute of Rural Development Planning (IRDP) – MwanzaREG/PWF/043Usajili KamiliUsajili Kamili
29Rungemba Community Development Institute (CDTI) – MufindiREG/PWF/007Ithibati KamiliIthibati Kamili
30Time School of Journalism (TSJ) – Dar es SalaamREG/PWF/013Ithibati KamiliIthibati Kamili
31COTC Machame – HaiREG/HAS/087Usajili KamiliUsajili Kamili
32Mwambani School of Nursing – ChunyaREG/HAS/089Usajili KamiliUsajili Kamili
33Kiomboi School of Nursing – IrambaREG/HAS/091Usajili KamiliUsajili Kamili
34College of Health Sciences ZanzibarREG/HAS/095Usajili KamiliUsajili Kamili
35Kabanga School of Nursing – KasuluREG/HAS/023Usajili KamiliIthibati ya Awali
36Kondoa School of Nursing – DodomaREG/HAS/040Ithibati ya AwaliIthibati ya Awali
37Lugarawa School of Nursing  – LudewaREG/HAS/036Ithibati ya AwaliIthibati ya Awali
38Tosamaganga School of Nursing  – IringaREG/HAS/020Ithibati ya AwaliIthibati ya Awali
39Vector Control training Centre – MuhezaREG/HAS/031Ithibati ya MudaIthibati ya Muda
40Training Centre for Health Records Technology – MoshiREG/HAS/072Ithibati ya MudaIthibati ya Muda
41Dar es Salaam School of Journalism (DSJ) – Dar es SalaamREG/PWF/012Ithibati KamiliIthibati Kamili
42Financial Training Centre – Dar es SalaamREG/BMG/004Ithibati ya AwaliIthibati ya Awali
Jedwali Na. 4: Taasisi na Vyuo vilivyoshushwa hadhi baada ya kutotimiza masharti ya Ithibati
Na.Jina la Taasisi/ChuoNamba yaUsajiliHadhi Kabla yaNotisiHadhi Baada yaNotisi
1Sura Technologies – Dar es SalaamREG/EOS/019Usajili KamiliUsajili wa Muda
2Institute of Management and Information Technology – Dar es SalaamREG/EOS/016Ithibati ya AwaliUsajili wa Muda
3Techno Brain – Dar es SalaamREG/EOS/021Ithibati ya AwaliUsajili wa Muda
4Ministry of Agriculture Training Institute Igurusi – MbeyaREG/ANE/009Ithibati ya AwaliUsajili wa Muda
5Mbozi School of Nursing – MbeyaREG/HAS/062Usajili KamiliUsajili wa Muda
6KCMC AMO Ophthalmology School – MoshiREG/HAS/085Usajili KamiliUsajili wa Muda
7KCMC AMO Anaesthesia School – MoshiREG/HAS/094Usajili KamiliUsajili wa Muda
8Advanced Pediatrics Nursing KCMC – MoshiREG/HAS/076Ithibati ya AwaliUsajili wa Muda
9AMO Training Centre Tanga – TangaREG/HAS/049Ithibati ya AwaliUsajili wa Muda
10CATC – SongeaREG/HAS/054Ithibati ya AwaliUsajili wa Muda
11CATC – SumbawangaREG/HAS/055Ithibati ya AwaliUsajili wa Muda
12COTC Maswa – ShinyangaREG/HAS/014Ithibati ya AwaliUsajili wa Muda
13COTC – MusomaREG/HAS/033Ithibati ya AwaliUsajili wa Muda
14Dental Therapists Training Centre – TangaREG/HAS/057Ithibati ya AwaliUsajili wa Muda
15Ngudu School of Environmental Health Sciences – KwimbaREG/HAS/058Ithibati ya AwaliUsajili wa Muda
16KCMC AMO General School – MoshiREG/HAS/096Ithibati ya MudaUsajili Kamili
Jedwali Na. 5: Taarifa kuhusu Taasisi na Vyuo vyenye maelezo maalum
Na.Jina la Taasisi/ChuoNamba yaUsajiliHadhi Kabla yaNotisiHadhi Baada yaNotisiMaelezo
1Lake Teachers College – SingidaREG/TLF/001Usajili wa MudaUsajili KamiliKimeruhusiwa kudahili wanafunzi
2Patricia Metzger Academy of Health and Beauty – Dar-es-SalaamREG/PWF/022PUsajili wa MudaUsajili wa MudaKimesitisha kutoa mafunzo
3Institute of Management and Entrepreneurship Development – Dar es SalaamREG/BMG/039Usajili KamiliUsajili KamiliKimesitisha kutoa mafunzo
4Tanga School of Nursing – TangaREG/HAS/084Ithibati KamiliIthibati KamiliHaijamaliza muda wa Ithibati
5ESACS School of Journalism and Business Studies – Dar es SalaamREG/PWF/044Usajili KamiliUsajili KamiliKimesitisha kutoa mafunzo
6Fire and Rescue Training Centre – Dar es Salaam.REG/EOS/032PUsajili wa MudaUsajili wa MudaKimesitisha kutoa kozi za muda mrefu. Sasa kinatoa kozi za muda mfupi ambazo hazipitishwi na Baraza (NACTE).
Asanteni kwa kunisikiliza.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
24 JUNI 2015