Sifurahishwi na uadui wa team za mitandaoni lakini sina nguvu ya kuzuia – Alikiba
Alikiba amekiri kutofurahishwa na uhasama unaondelea kati ya mashabiki wake na mashabiki wa Diamond Platnumz kwenye mitandao ya kijamii japo amesema hana uwezo wa kuzuia hali hiyo.
- “Unajua sisi ni vioo vya jamii na tunapendwa na watu wengi sasa unapoona mambo yanatokea kama hivyo huwezi kufanya chochote na mimi siwezi kuingilia suala lolote la mashabiki,” Alikiba amekiambia kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM.
- “Lakini kiukweli sifurahishwi nalo kama kuna uwezekano wangeacha tu. Kiukweli tusupport vya kwetu ili tuwende kwenda mbele.”