Friday, July 10, 2015

WATAZAME MASTAA WADOGO ‘VISU’ WALIOTIKISA WAKONGWE!

Staa wa Bongo, Wema Sepetu.
Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Na Mwandishi wetu
Kama wewe ni mfuatiliaji wa mambo utakubaliana na mimi kwamba, wapo mastaa wa kike ambao wana maumbile madogo na umri wao ni mdogo pia lakini ni wakali ‘visu’ kiasi cha kuwakosesha amani mastaa wakubwa.
Yaani kimaumbile unaweza kusema ni watoto flani hivi lakini cha ajabu mambo yao ni makubwa na wanamudu kuwaweka viganjani wanaume wenye midevu yao na wakatulia.
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Umenipata? Kama bado, iko hivi, unamjua vizuri binti anayefahamika zaidi kwa jina la Lulu? Hapa namzungumzia Elizabeth Michael! Je, unamfahamu bishosti anayeitwa Husna Maulidi? Tunda Sabasita, almaarufu kama Tunda je?
Kama jibu ni ndiyo, mabinti hawa ni tishio mjini! Ni wazuri, wanajua kuwavuta wanaume na ni wajanja wanaojua kuwatumia wanaume vizuri.
Na kwa taarifa yako sasa mastaa wengine wakiwemo wakongwe wanaowaonea gere sana kwani wamo waliowahi kutikiswa kwenye himaya zao.

Lulu vs WemaHusna Maulid.
Historia inaonesha kuwa, Lulu aliwahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na marehemu Steven Kanumba. Lakini wafuatiliaji wa mambo ya watu wanaeleza kuwa, Kanumba alimtosa Wema na kuhamia kwa Lulu kisha penzi likawa la siri?


Je, ulitarajia siku moja mwanaume kama Kanumba kumuacha Wema anayeonekana ni bomba na kuhamia kwa Lulu? Jibu baki nalo lakini ukweli ni kwamba licha ya udogo wake Lulu alimzidi kete ‘dada’ yake, Wema!
Jacqueline Wolper.
Husna vs Wolper
Unakumbuka Husna aliwahi ‘ku-date’ na mwanaume aitwaye Radjabu Mwami (Mkongo)? Cha ajabu sasa Wolper naye akaenda kujiweka kwa mwanaume huyo, alipogundua kuwa anashea penzi na dogo, akaamua kumwaga manyanga. Katika hali ya kawaida Wolper ni wa kumuachia Husna mwanaume? Jibu ni kwamba alijua akikomaa, yeye atakuwa wa kwanza kuachwa kwa kuwa Husna ni kisu zaidi yake.
Agnes Gerald 'Masogange'.
Tunda vs Masogange
Tunda ni binti mdogo sana na siyo staa kivile lakini aliweza kuvamia himaya ya Video Queen Masogange na kumfanya modo huyo aliyejaaliwa kuwa na kalio kubwa atoswe na yule mwanaume wake wa Sauzi aliyekuwa akimpa maisha huyo.
Kuna siri gani hapa?
Ukweli ni kwamba Lulu, Husna na Tunda wana ‘baby faces’ lakini ni watundu wanaojua kujiweka vizuri kiasi cha kuwatishia nyau wakubwa zao. Ndiyo maana akisimama Lulu na Wema, kwa mwanaume anayetaka msichana kwa maana halisi ya msichana atamchukua Lulu. Vilevile kwa Tunda na Masogange, Husna na Wolper.
Hata hivyo, bado ukweli unabaki palepale kwamba kinachowabeba akina Lulu ni ule usichana wao lakini Wema, Wolper na Masogange ni habari nyingine wewee! Wametingisha kwa uzuri tangu miaka hiyo na mpaka leo bado wamo na mvuto wao hauchuji. Kama huamini katika hilo, subiri Shindano la Ijumaa Sexiest Girl 2015 litakaloanza hivi karibuni uone kazi!