Tukio hilo la kustaajabisha lilitokea saa mbili usiku wakati vijana hao wakicheza kamari ambayo dau lake lilikuwa Sh. 200.
KIJANA aliyejulikana kwa jina la Julius Matiko Makenge , mkazi wa Kitunda Kivule jijini Dar amedaiwa kuawa kwa kuchomwa kisu na rafiki yake wa karibu aitwaye Josephat maarufu kwa jina la Chaga, kisa kikidaiwa kuwa ni kuliwa Sh. 200 wakati wakicheza kamari.Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa sababu za kiusalama, wakati wakiendelea kucheza, ilifika zamu ya Julius baada ya kuliwa kiasi hicho cha fedha hakuridhika hivyo aliendelea kudai fedha yake (Sh. 200) bila mafanikio, ndipo ugomvi uliibuka kati yao hadi kusababisha kifo chake.
“Josephat ambaye ni muuza duka alipoona madai yanazidi aliingia dukani kama mtu aliyekwenda kumhudumia mteja kumbe alifuata kisu ambacho alikificha mfukoni bila mtu kujua kisha alikitumia kumchoma nacho tumboni Julius,” alisema shuhuda huyo.
Mmoja wa wasemaji wa familia ya marehemu, aliyejitambulisha kwa jina la Marwa alisema Julius alifika kwao kwa ajili ya kutoa taarifa juu ya tukio hilo ambapo alimkuta baba yake mzazi na kumwambia aliyemchoma kisu anaitwa Josephat.
Alisema kuwa baada ya taarifa hizo, wanafamilia walianza kufanya taratibu za kutafuta gari kwa ajili ya kumpeleka hospitali lakini hawakufika umbali wa mita 500 akafariki dunia baada ya kutokwa damu kwa wingi kwenye jeraha.
Aliongeza kuwa familia ilishangazwa na tukio hilo kwani marehemu na muuaji walikuwa ni marafiki wakubwa.
Kwa mujibu wa taarifa za kipolisi ambazo zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, SACP Lucas Mkondya, Josephat tayari anashikiliwa na polisi baada ya kukamatwa akiwa Mombo, mkoani Tanga.
Mazishi ya marehemu yalifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Makaburi ya Kanyigo Kitunda.: