Tuesday, September 15, 2015

IRENE UWOYA AFUNGUKA MAZITO,AWAPA MAKAVU WASAANI HAWA KISA KIKWETE


Irene Uwoya 
Staa wa Bongo Movies, Irene Uwoya ambaye ameshapitishwa na chama chake cha CCM kuwania ubunge wa viti maalum amewapa makavu baadhi ya wasanii wenzake wa bongo movies ambao hawakiungi mkono chama cha mapinduzi wakati baadhi yao walikuwa karibu sana na Rais Kikwete anaye maliza muda wake. 
Kupitia kurasa wake kwenye mtandao picha wa instagram, Uwoya awachana wa sanii hao kuwa yule wa nao muunga mkono hakuwahi kuwathamini hata siku moja. 
"Sasa narudi kwa wasaniii wasio jitambua!katika tasnia yetu ukweli usio pingika Mh.Kikwete amekuwa karibu Sana na wasaniii na ametufanya tudhaminike.
Lakini chaajabu kunawatu wanajifanya hawajui mchango wake, kiukweli inaumiza sana! 
Kunawatu walikuwa wanashinda Ikulu na Mh, anawasaidia sana katika kazi zao lakini leo wamesahau yote na kumsapot mtu ambaye hajawahi hata kuwatambua kwanafasi zao, kama sio ushabiki maandaz niniii? Loooo!!!aibu".Uwoya aliandika.