MCHEKESHAJI wa kundi la Orijino Komedi, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’, amewataka wanaomtuhumu kwamba anatumia tiketi ya uchungaji kama njia ya kujiingizia kipato wajaribu kazi hiyo wataona malipo yake.
Aliongeza kuwa uchungaji ni wito na siyo kazi, pia uchekeshaji ni ajira yake, hivyo hawezi kuacha uchekeshaji kwa sababu ya uchungaji kwa kuwa hakiuki miiko ya uchungaji.
“Eti wanasema uchungaji na siasa wapi na wapi, mbona kuna chama cha siasa kimojawapo mgombea wao wa urais ameletwa na mchungaji lakini kwangu ndiyo siyo sawa? Anayedhani uchungaji ni dili, ajaribu aone kama hajatoka majipu kama Ayubu,” alieleza Masanja, alipokuwa katika moja ya mikutano ya kampeni ya kisiasa alipoalikwa na Chama Cha Mapinduzi.
Chanzo: Mtanzania