HEE! Staa kiwango kunako tasnia ya filamu Bongo, Aunt Ezekiel hivi karibuni alishindwa kupata usingizi kufuatia kuangua kilio sababu ikiwa ni kumkumbuka mtoto wake, Cookie ambaye hajamuona kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa kutokana na kubanwa na misafara ya kampeni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza kwa uchungu, Aunt alisema, japokuwa yupo kwenye kampeni hizo lakini kila wakati anamkumbuka mtoto wake kwa kuwa alimuacha muda mrefu na yeye akiwa kama mama mwenye uchungu lazima ifike wakati amkumbuke mtoto wake huyo.
“Mara nyingi sipati usingizi kwa kumuwaza Cookie. Kama leo sijalala kabisa, nilikuwa nalia kwa ajili yake. Nimemkumbuka sana mwanangu. Hii yote ni kwa ajili ya kazi na kumtafutia maisha bora ndiyo maana nikaamua kumuacha na baba yake,” alisema Aunt.