Thursday, October 1, 2015

Faiza: Tuwe Tunahofu ya Mungu, Wanaomponda Lowassa na Ugonjwa Wake na Wema Kutopata Mtoto

Saa nyingine ili uone uzito wajambo inabidi
uvae viatu vya mwenzio- kwa kweli imefika wkt
najisikia vibaya kuhusu kusoma ugonjwa wa
LOWASA, watu wameona ndio fimbo ya
kumchapia kuhusu ugonjwa wake kwa kweli
sijisikii vizuri na sioni kama sawa
Pia katika pita pita huku insta nimeona Wema
na mbwa na Zari na mtoto na maneno ya
kashfa juu yake, jamani watanzania
mnamatatizo gani kuhusu maisha ya watu!
Kwa nini unamsema vibaya mtu juu ya kilema
chake ? Kwa nini usimsema mapungufu yake
bila kumkashifu juu ya marazi au kilema ? Hii
ni sawa kweli? .
Nakumbuka kuna wakati watu walinisema sana
kuhusu ukimwi! Nikawa najiuliza hii ingekua
kweli na ukimwi ingekuaje ningejisikiaje tena
kuna watu walikua wana nitukana live ikiwemo
na kumwambia mtu ambae niko kwenye
mahusiano nae, hivi mnazani kuna mtu
ameomba marazi kweli.
Nyinyi mnaosema watu kuhusu vilema vyao je
mnajua mnawaweka watu kwenye wakati
gani?, hivi unajua kwa kumuandama mtu
unaweza ukamuua au kumuongezea matatizo
na saa nyingine kuchukua hatua mbaya.
Unae msema mtu unataka kuwa sababu ya
matatizo yake ? Kama ni hapana basi tafazalini
jamani tusemane yote lkn sio kwa mambo
kama marazi au ugumba au kilema- jamani
kabla hujafa hujaumbika tumuogope MUNGU
tuwe tunahofu ya MUNGU
Faiza Ally @faiza_ally on Instagram