Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM, January Makamba ameonesha kutokubaliana kwake na ripoti za kinachojili kwenye mikutano ya mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa na kueleza kuwa Magazeti hutumiwa kupiga kampeni.
Makamba ameeleza hayo kupitia mtandao wa Twitter baada ya mtu mmoja anaetumia jina la ‘Gachanja Muigai’, kumueleza kuwa kutokana na kile wananachokisoma, inaonekana kuwa wananchi wengi wanamuunga mkono Lowassa. Na akataka kupata maoni ya Makamba kutokana na hali hiyo kama anadhani wataweza kushinda.
“@JMakamba @MagufuliJP From what we read here, it seems #Lowassa is resonating with Wananchi. Una hakika si wakati wa kuvuka sakafu?” Aliuliza.
Makamba alimjibu kuwa wapinzani wanatumia baadhi ya magazeti kama sehemu ya kampeni zao lakini tafiti na hali halisi nchini inaeleza tofauti.
“They’ve turned some newspapers into their campaign fliers. But the polls & mood across Tanzania tell another story.”