MWALIMU wa kike nchini Marekani,
Michelle Sulzicki (28) anadaiwa alifanya ngono zaidi ya mara 20 na
mvulana mdogo mwenye umri wa miaka 12, ambapo mvulana huyo hivi sasa
anahofu kwamba mtoto aliyezaa mwalimu huyo ambaye sasa ana umri wa miezi
mitano ni wa kwake.
Katika kufanya uchunguzi, polisi
wamesema kwamba mwalimu huyo aliyekuwa akifundisha katika Shule ya
Msingi ya Stratford, Jimbo la Connecticut, alifanya ngono kwa siri na
mvulana huyo kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu.
Vilevile, katika ripoti iliyotolewa na
vyombo vya habari, mvulana huyo aliwaambia walimu wake kwamba yeye na
Michelle Sulzicki walifanya ngono kiasi cha mara 20, ikiwa ni pamoja na
ngono ya kutumia midomo, na ngono ya kinyume na maumbile.
Mvulana huyo anatarajiwa kufanyiwa
kipimo cha kugundua iwapo ndiye baba wa mtoto wa kike aliyezaliwa na
mwalimu huyo. Hilo limekuwa ni lazima kwa vile polisi walisema wawili
hao walifanya ngono bila kutumia kinga (kondom).
Kwa mujibu wa gazeti la Daily News,
mwanafunzi huyo alifichua udhalilishaji huo aliofanyiwa kwa kuwaambia
walimu wake akiwa kwenye shule yake mpya baada ya kuondoka katika Shule
ya Msingi ya Stratford, huko Connecticut.
Mwanafunzi huyo aliwaambia wachunguzi wa
tukio hilo kwamba Sulzicki, 28, alikuwa akimvutia kwa kumpa zawadi
mbalimbali, lakini aliripoti tukio hilo la kudhalilishwa akiwa anahofia
kwamba huenda alimpa ujauzito, liliandika gazeti la Connecticut Post.
Wakati akijisalimisha kwa polisi jana,
mwalimu huyo, alikana madai hayo dhidi yake lakini baadaye alikiri
kufanya ngono na mvulana huyo mara moja tu.
Sulzicki anashitakiwa kwa makosa mawili ya shambulizi la ngono na kufanya ngono na mtoto mdogo.