Video Queen Tunda Sabasita.
Video Queen Tunda Sabasita hivi karibuni ameweka wazi uhusiano wake wa kimapenzi na mwanamuziki David Genze ‘Young D’ ambapo amesema Mungu akipenda ndoa yao itafungwa soon.
Mwanamuziki David Genze ‘Young D’.
Akiongea na Ijumaa, Tunda alisema kuwa ni kweli yuko katika kisiwa
cha mapenzi na mwanamuziki huyo na kuweka wazi hisia zake kuwa anampenda
sana na kumthamini tofauti na watu wanavyo muongelea.“Ni kweli niko na D na ninampenda sana, Mungu akipenda tutakuwa mwili mmoja soon kwa sababu nimempima na kuona ndio mwanaume mwenye nafasi kubwa kwenye moyo wangu,”alisema Tunda.