Akistorisha na gazeti hili wikiendi iliyopita, Gigy alisema kwa kuwa anatafuta fedha ya kubadili maisha yake, anaweza kufanya tendo hilo kwa sababu anahitaji kuishi kitajiri zaidi.
Aliendelea kusema kuwa amewahi kufuatwa na watu mbalimbali kutoka Dubai wakimtaka kwenda kucheza filamu hizo, lakini alikataa kutokana na fedha walizomtajia kuwa ni kidogo na hakuwa tayari kwa muda huo.
“Yaani nikiambiwa napewa mamilioni nicheze picha hizo nipo tayari maana hapa duniani wanaokula starehe zaidi ni wale wenye fedha sasa nikipewa mamilioni ili nibadili maisha yangu, niko tayari maana nitabadili maisha yangu na nitaishi kitajiri hapo mpaka watu waje kunishtukia nitakuwa nimeshakula bata vya kutosha,” alisema Gigy.
Gigy Money ni miongoni mwa ma-video Queen chipukizi wanaofanya vizuri katika video za wasanii wa muziki wa kizazi kipya.
Chanzo:GPL