MUIGIZAJI mwenye mvuto wa aina yake katika tasnia ya filamu Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ amempa somo mshindi wa Shindano la Tanzania Move Talent ‘TMT,’ Mwanafaa Mwinzago kuwa asibweteke na ushindi aliopata bali azingatie masomo.
Muigizaji mwenye mvuto wa aina yake katika tasnia ya filamu Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’.
Akizungumza na Ijumaa juzikati, Lulu alisema ni kweli binti huyo ana kipaji na ilikuwa haki kushinda milioni 50 ila ajue bado ni mtoto na anatakiwa kukomalia elimu.
“Ustaa ni cheo kikubwa sana hasa katika jamii na kila mtu anakuangalia wewe, ili ujikontroo unatakiwa ujitambue na huwezi kujitambua kama huna elimu ya kutosha hivyo mimi namshauri aweke suala la masomo mbele kuliko ustaa alioupata,” alisema Lulu.
Fainali za TMT zilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Ukumbi wa Mlimani City ambapo Mwanafaa aliibuka kidedea.