Friday, September 5, 2014

BAADA YA KUSIKIA KAJALA ANA PESA CHAFU, MUMEWE AMBYE YUKO JELA AFUNGUKA HIVI

ANA hoja? Siku chache baada ya gazeti pacha la hili, Ijumaa Wikienda, toleo la Jumatatu iliyopita kuripoti juu ya utajiri mkubwa wa staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘K’, mumewe Faraji Agustino amempigia saluti na kumuomba amtoe gerezani.
Kajala na mumewe wakiwa mahakamani.
KWANI ILIKUWAJE?
Machi mwaka jana, Faraji alihukumiwa kifungo cha miaka saba jela au faini ya zaidi ya Sh. milioni 200 baada ya kupatikana na hatia ya kutakatisha fedha haramu kwenye Benki ya NBC, Tawi la Dar ambapo jamaa huyo alishindwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kujikuta ‘akiozea’ Segerea au Segedansi kama wanavyoita mastaa wa Kibongo.
UTAJIRI WA GHAFLA
Katika msala huo, Kajala alihukumiwa miaka mitano jela au faini ya Sh. milioni 13 kwa kukutwa na hatia ya kuuza nyumba yao iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ambapo alilipiwa shilingi Milioni 13 na Wema Isaac Sepetu na sasa anapeta mtaani na utajiri wa ghafla.
HOJA YA MSINGI
Baada ya kuokolewa jela na Wema, Kajala ametembelewa na utajiri ambapo amekuwa akitanua mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar, akisukuma magari ya kifahari, kupanga ghorofa maeneo ya Sinza-Madukani anayolipia Sh. milioni 3.2 kwa mwezi, akimiliki kampuni ya kuzalisha sinema ya Kay Entertainment huku akaunti yake ikiwa imenona kwa mamilioni kadhaa.
GEREZANI SEGEREA
Hivi karibuni, ‘mtu wetu’ alikwenda kumtembelea Faraji kwenye Gereza la Segerea, Dar ambapo alipata nafasi ya kutoa la moyoni juu ya mkewe Kajala ambaye alifunga naye ndoa kanisani miezi michache kabla ya kukutwa na msala huo.
Akizungumza kwa huruma, Faraji alisema habari za Kajala kuwa na utajiri wa kutupwa alianza kuzisikia kwa ndugu zake hivyo kumuomba staa huyo kumkumbuka kwenye ufalme wake.
Kajala na mumewe siku ya ndoa.
Jamaa huyo alisema kila akikaa huwa anakumbuka good time (kipindi cha matanuzi) yao ambapo ilikuwa ni bata mwanzo mwisho hasa nyakati za wikiendi.
Kwa mujibu wa mtu wetu huyo, Faraji alimwambia: “Mwambieni K akumbuke yeye ni mke wangu. Nimemsaidia kwa mengi, asiniache nateseka huku yeye anachezea pesa ambazo anaweza kunilipia na nikatoka kifungoni. Pia akumbuke ahadi yetu ya ndoa kanisani na jinsi tulivyoishi kwa upendo.
“Bado ni mke wangu, bado nampenda sana. Nilisikia alishavua pete ya ndoa lakini ukweli ni kwamba bado mapenzi yetu yapo palepale. Kama kweli Kajala amepata utajiri naomba anitoe gerezani, sitamsahau maisha yangu yote. Kama nilivyoahidi kanisani, nitampenda na kumtunza hadi kifo kitutenganishe.”
Chanzo hicho kilidai kwamba Faraji alisema Kajala amuonee huruma, azungumze na wadau wake wote wamtoe gerezani halafu atajua jinsi ya kurejesha fedha hizo.Habari nyingine kuhusu suala hilo ilisemekana kwamba jamaa huyo ametengeneza netiweki akiwa gerezani kupitia kwa watu wake wanaomtembelea ambao wapo tayari kuungana na staa huyo ili kufanikisha jambo hilo.
Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘K’.
INAWEZEKANA?
Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa wanasheria wenye uzoefu na kesi za mastaa aliyeomba hifadhi ya jina alisema kwamba jambo hilo linawezekana endapo mteja (mume wa Kajala) ataomba kesi yake ifanyiwe ‘reference’ (mapitio).
“Unajua haya ni mambo ya kisheria, kwa mtu wa kawaida anaweza asiyaelewe kirahisi lakini uwezekano upo bila hata kukata rufaa.“Faraji alihukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu (Dar). Kitakachofanyika ni kwamba kama akitaka kesi yake itafanyiwa reference kwenye mahakama ya juu.
“Baada ya hapo Faraji au wakili wake anaweza kuomba kulipa faini badala ya kifungo kwa sababu hukumu ilisema kifungo cha miaka saba au faini ya hiyo shilingi milioni 200.
“Kama kweli Kajala ana hiyo fedha si mbaya akafanya hizo process (taratibu), akamtoa mumewe,” alisema ‘loya’ huyo.
KAJALA ANASEMAJE?
Baada ya kujazwa data hizo, Jumatano iliyopita Ijumaa lilimtafuta Kajala ambaye simu yake haikuwa hewani kila ilipopigwa na hata alipofuatwa nyumbani kwake hakuwepo lakini kwenye makabrasha kulikuwa na maelezo yake juu ya mumewe alipohojiwa siku kadhaa zilizopita.
Kwa mujibu wa Kajala, Faraja bado ni mumewe na huwa anakwenda gerezani kumuona kila wikiendi na anatamani awe huru ili waendelee na maisha kwani hawakuwa wamefaidi penzi lao, hata mtoto walikuwa hawajapata.
MARAFIKI WANASEMAJE?
Marafiki wa wanandoa hao waliozungumza na Ijumaa walisema kwamba kama kweli Kajala ana nia hiyo, basi afanye hiv yo kwani itakuwa thawabu kubwa kwake kama alivyofanyiwa na Wema aliyemnusuru kifungo cha miaka mitano jela.